Serikali imesema kuwa uamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kutokutangaza Shule bora kwa kutegemea matokeo ya mwisho ya mitihani ni kwa sababu ya utata wa namna ya kutathmini Shule bora.

Ufafanuzi huo wa Serikali umetolewa Bungeni leo Jumatano (February Mosi) na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda baada ya mwongozo ulioombwa Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Mwita Getere.

Prof Mkenda ametoa mfano kuwa Shule yenye Wanafunzi 100 na nyingine ina Wanafunzi 20 waliomaliza kidato na nne, ya Wanafunzi 100, 70 wamepata A, 30 hawakupata A na yenye Wanafunzi 20 wote wamepata A, kwa kuangalia wastani wa ufaulu yenye Wanafunzi 20 itatangazwa kuwa Shule bora lakini wengine wanaweza kuona yenye Wanafunzi 70 wenye A ndio iwe Shule bora.

Prof. Mkenda amesema aina hiyo ya tathmini inaweza kupelekea shinikizo kwa Shule yenye Wanafunzi mathalani 100 kwa kuondoa wale 30 ambao hawakupata A ili iweze kutangazwa Shule bora kwa kupata A zote ambazo ni asilimia 100.

Mkenda amesema kuwa takwimu zote zipo hadharani lakini Baraza limejiondoa kwenye jukumu la kutangaza na hazijafichwa takwimu za matokeo ya Shule zote na ufaulu wake zipo.

Kocha Bares asaini mmoja Tanzania Prisons
GGML yatoa mafunzo kazi kwa wahitimu vyuo vikuu