Shule ya sekondari ya Almutanzir iliyopo upanga jijini Dar es salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini zinazotakiwa kisheria.

Faini hiyo imetakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Luhaga Mpina iliyofuatia baada ya malalamiko ya wakazi wa Upanga.

Aidha, meneja wa shule hiyo  Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea swala la ukuta wa shule hiyo.

Naibu waziri amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekezaji watakaokiuka sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.

Hata hivyo Naibu Waziri ametembelea maeneo  ya mwenge kijijini na kujionea uchafu wa mazingira unaotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo ya mwenge hali ambayo  inahatarisha maisha na kupata magonjwa ya maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.

Naibu Waziri Mpina ameitaka NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.

Serikali kuchukua rasmi shamba la Sumaye, 'hatuangalii sura ya mtu'
Video: Makonda atoa maamuzi mazito kuhusu Machinga Dar