Shule za awali, Msingi na Sekondari za Atlas zinazomilikiwa na Atlas Marc Group zimedhamiria kuboresha huduma zao katika utoaji wa elimu nchini lengo likiwa ni kuongeza matokeo mazuri pamoja na kuwajenga wanafunzi wanaomaliza katika shule hizo kupata misingi mizuri itakayowasaidia maishani.
Mkuu wa kitengo cha shule za awali kilichopo  Madale, Sarah Namkwahe amesema kuwa katika muhula huu wametambulisha zoezi la kujenga kujiamini miongoni mwa wanafunzi hao wa awali.
Namkwahe amesema licha ya kumjenga mtoto katika kuboresha matumizi ya lugha zote mbili za kiingereza na kiswahili lakini pia kujieleza mbele ya wenzake darasani kunamjenga mwanafunzi kujiamini wakiwa mdogo.
“Hii itawafanya kuwa wanafunzi bora hata katika masomo yao ya mbele lakini vile vile kuwa watu wenye mafanikio maishani” anasema Mkuu wa kitengo cha awali.
Pia uongozi wa shule hizo umetambulisha zoezi la kusoma mashairi na kuhadithia hadithi mbali mbali ili kuwafanya watoto kuwa na uelewa wa mambo mbali mbali na kujifunza pia.
Shule ya awali inayo jumla ya watoto 245 ambapo wa kiume ni 132 na kike ni 113 ambao madarasa yao yamegawanyika katika mikondo sita ikiwemo ile ya awali ya wadogo kabisa, darasa la chini, madarasa mawili ya kati kati  na darasa la juu la A na juu zaidi.
Mwalimu wa shule ya Msingi  hapo Madale, Sarah Nalubega amesema katika shule za msingi mikakati waliyonayo ni  kufundisha  kwa bidii kupitia  walimu wao waliobobea, pia kumekuwa na mazoezi ya mara kwa mara hasa kwa madarasa ya juu ya la sita na saba ambao wanatarajia kufanya  mitihani yao mwezi Septemba mwaka huu.
Hata hivyo  amesema wamekuwa na utaratibu wa kuwapa wa kuwashauri wanafunzi wanapokuwa na changamoto mbali mbali za kimaisha kwa vile kila mmoja anatokea katika maeneo tofauti ili kuwafanya kuwa kitu kimoja na kujiona wanaweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 30, 2019
Video: MacLeans BeneCIBO yawaneemesha wakulima kimasoko