Baraza la mitihani la taifa NECTA, limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2020 ambapo shule za serikali zimengara katika nafasi 10 bora.

Matokeo hayo yametangazwa leo Agosti 21,2020 na katibu mtendaji wa NECTA Dkt Charse Msonde visiwani Zanzibar.

Katika shule kumi bora kitaifa kwenye matokeo hayo nane zinamilikiwa na serikali na mbili ni shule binasfi, shule ya Kisimiri Sekondari yenye idadi ya watahiniwa 53 iliyopo mkoani Arusha imesalia kuwa nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa mwaka 2019.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 22, 2020
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 21, 2020