Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji amekanusha kuhusika na ujumbe uliondikwa kwenye ukurasa wake Instagram uliokuwa ukiponda utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusema kuwa hakubaliani nao.

Shyrose amesema kuwa ukurasa wake huo ulikuwa umedukuliwa na watu wasiojulikana hivyo, hahusiki chochote na kilichoandikwa kwenye ukurasa huo.

“Namuomba radhi Rais wangu, Dkt. Magufuli na wote waliokwazika na ujumbe huo, akaunti yangu ilikuwa imedukuliwa na watu wasiojulikana,”ameandika Shyrose kwenye ukurasa wake

Bondia afariki dunia baada ya kushinda pambano
Sugu, Masonga wafungwa miezi mitano jela