Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka kuhusiana na Mwenyekiti wake, Dkt. John Magufuli kuwateua viongozi wanachama wapya waliotoka upinzani, ambapo amedai kuwa CCM haitazami historia ya mtu.

Amesema kuwa si kila mwanachama wa CCM anasifa za kuwa kiongozi kwani kazi ya chama ni kuandaa raia wema na wanachama waaminifu.

“Chama cha Mapinduzi kina zaidi ya wanachama milioni 12-14, hivyo basi kwa wingi huo haiwezekani wote tukaingia kwenye chama tukiwa na fikra ya uongozi, cheo ni dhamana na kila mwana CCM ana haki sawa za kupata nafasi ya uongozi, ukishakuwa kuwa mwanachama wetu hatutazami historia tunachotazama ni vigezo vya uongozi,” amesema Polepole.

Aidha, hayo yamejiri baada ya Rais Dkt. Magufuli, Julai 28, 2018  kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao,  huku akiteua wanasiasa waliotokea vyama vya upinzani.

Walioteuliwa ni pamoja David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali (Kasulu Mjini, NCCR Mageuzi), na Patrobas Katambi (aliyekuwa mwenyekiti Baraza la Vijana la Chadema, wote wakiwa wamejiunga na CCM kati ya mwaka jana na mwaka huu.

Hofu ya 2018/19 yamvuruga Mourinho, asema na uongozi
Axel Tuanzebe, Demetri Mitchell kuondoka Old Trafford