Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kuzungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga leo Agosti 23, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Kamishna Sianga amemhakikishia Rais Magufuli kuwa kazi ya kukabiliana a na tatizo la bishara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.

Amesema kuwa tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni Bangi, Heroine, Cocaine, Kemikali Bashirifu na kwamba kwa sasa wameanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.

Pia, Kamishna huyo amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi na sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya, pia mamlaka hiyo itatoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya.

Aidha, ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kuelvya kuwapeleka katika mamlaka hiyo ili watibiwe.

ma1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Rogers Sianga alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.

ma2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya Rogers Sianga alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 23, 2017.

 

Video: Simba yaikaanga Yanga, yatwaa ubingwa kombe la Ngao ya Jamii
Chadema yapata pigo tena, yakimbiwa na madiwani wengine