Kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa hana uhakika kama atakutana na Kocha wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho kwakuwa anaachana na timu hiyo.

Ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Manchester United na Arsenal uliopigwa katika dimba la Old Traffod huku Manchester United ikiibu na ushindi wa goli 2- 1.

Katika mechi hiyo iliyochezwa siku ya jumapili, United walitangulia kupata bao dakika ya 16 kupitia kwa Paul Pogba, huku Henrikh Mkhitaryan akiisawazishia Arsenal dakika ya 51.

“Nimefanya kazi ya ukufunzi kwa muda wa miaka 34, bila kupumzika na nadhani kwasasa mimi ndiye kocha aliyefundisha kwa muda mrefu bila kupumzika,”amesema Wenger

Aidha, akimzungumzia kocha wa United, Wenger kuwa hana uhakika kama atakutana naye katika msimu ujao kwani mpaka sasa hajui kama ataendelea kufundisha timu ama la.

Hata hivyo, kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson kabla ya kuanza mchezo huo alimkabidhi zawadi Mfaransa huyo.

 

 

Familia ya Heche yagoma kuuzika mwili wa nduguye
Polepole ashangazwa ACT-Wazalendo kuendeshwa mtandaoni

Comments

comments