Saa kadhaa kabla ya watanzania kushiriki katika zoezi la kihistoria la kupiga kura kumchakua Rais wa Serikali Ya Awamu Ya Tano, ushindani mkubwa kati ya wagombea urais wa CCM, Dkt. John Magufuli na wa Chadema, Edward Lowassa unaendelea kuonekana huku hali ikiwa ngumu kumtabiri mshindi moja kwa moja.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa kimataifa waliofanya mahojiano katikati ya mwezi Oktoba wameeleza kumpa nafasi kubwa zaidi ya ushindi Edward Lowassa, huku tafiti zilizofanywa ndani na Taasisi zisizo za kiserikali za Twaweza na IPSOS zikimpa nafasi zaidi Dkt. John Magufuli.

Twaweza na IPSOS kupitia matokeo ya tafiti zao yaliyotolewa siku takribani 30 zilizopita, yalionesha kuwa Dkt. Magufuli atashinda kwa kwa kishindo zaidi ya aslimia 60 dhidi ya Lowassa ambaye alipewa silimia chini ya 30.

Kwa mujibu wa Twaweza, Dkt. Magufuli angeweza kushinda kwa asilimia 66 huku Lowassa akipewa asilimia 25 endapo uchaguzi ungefanyika kabla ya Septemba mwaka huu.

Wakati tafiti hizo zikionesha kumpa nafasi zaidi Dkt. Magufuli, baadhi ya wachambuzi wa kimataifa wa masuala ya siasa walimpa nafasi kubwa zaidi Bw. Lowassa.

Akiongea katika kipindi cha Straight Talk Afrika, cha Sauti ya Amerika (VoA), Profesa Nichollos Boas Forsees alisema kuwa kutokana na mwenendo wa kampeni na takwimu zilizotolewa na serikali, Lowassa ana nafasi kubwa zadi ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

“Kuna uwezekano mkubwa kwamba Lowassa atashinda,” alisema Profesa Nicholls Boas Forsees kisha kutoa mchanganuo wa mawazo yake.

“Nitakwambia kwanini, Kuna takwimu kutoka serikalini zinazoonesha kuwa kati ya watu wenye umri wa miaka 18 hadi 25 ni vijana, na kati ya 25 na labda kufikia miaka 70 hawa ni watu wazima. Kwa kawaida hawa watu wanaonesha, hususan vijana wengi ambao wanaitwa ‘bodaboda’ na watu wa Bajaji watapiga kura kuhakikisha biashara zao zinalindwa, na Lowassa ameingia kwao na inaokana kuwa kuna mwitikio mkubwa wa watu wanaomuunga mkono Lowassa. Na unaweza kuona pia kwa kutumia njia ya utafiti ya kuangalia (observation research method), unaweza kuona Lowassa anapata umati mkubwa sana. Sijasema Magufuli hapati [umati]. Lakini inaonekana kama Lowassa yuko katika wakati ambao anavuta watu wengi zaidi ya Magufuli. Na ujumbe wa Lowassa unawagusa watu hao. Tatizo la Magufuli na CCM, ujumbe wao haivutii kwa mantiki kuwa kuna mengi ambayo walikuwa wameahidi lakini hawakuyatekeleza.”


Hata hivyo, tafiti na uchambuzi vitabaki kuwa maoni tu kwa kuwa uhalisia utadhihirika baada ya zoezi la kupiga kura, kuhesabu kura na kumtangaza mshindi.

Super Sunday, Man Utd Vs Man City
Lionel Messi Awakana Mashabiki Maandazi