Muda wa siku tatu umeongezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania  (NEC) katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoa wa Dar es Salaam uliotarajiwa kufikia ukomo wake leo alhamisi februari 20,2020.

Uboreshaji huo wa daftari ulianza februari 14,2020 na leo ijumaa ya februari 20,2020 ndio ulikuwa mwisho lakini tume hiyo imeongeza siku nyingine tatu kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria 15(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura namba 343 pamoja na sheria ya uchaguzi wa Serikali za mitaa sura namba 292.

Mkurugenzi wa tume hiyo Dk Wilson Charles amewataka wakazi wa mkuo huo kutumia vyema mda uliongezwa na Tume.

”Kwahiyo ikifika tarehe 23,2020 siku ya jumapili hatutaongeza muda tena”amesema Dk Charles

Kwa mujibu wa tume hiyo vituo 37,814 vitatumika katika uboreshaji wa daftari hilo kwa Tanzania bara na visiwani.

Nzige wageuzwa chakula Uganda
Lamar Odom ajutia kuukataa ushauri wa Jay-Z

Comments

comments