Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ametangaza kuanza kuchukua hatua za kuwafutia leseni mawakala wote wanaouza saruji kwa bei ya juu licha ya kutokuwapo kwa upungufu wa bidhaa hiyo kwa sasa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Tanzania Portland Cement (Twiga)  kilichopo Wazo na Camel Cement Company kilichopo Mbagala.

Hatua hiyo imekuja mara baada kutengemaa kwa mitambo ya uzalishaji malighafi ya saruji katika viwanda kadhaa nchini ambao ulisababisha uhaba wa saruji sokoni kwa zaidi ya siku 20.

Aidha, Mwijage amesema kuwa lazima baadhi ya mawakala wanaouza saruji ei juu watolewe kafara ili kudhibiti hali hiyo.

“Suala hili la saruji kupanda, naomba watu wanivumilie, dawa ya kupanda naijua, saruji imejaa sokoni, bei inashuka yenyewe, ila wale wanaopandisha inaitwa ‘profiteering’ siku ya kiama inshallah basi hukumu ni yao kama wanataka kuishi duniani shauri yao hukumu ni yao,”amesema Mwijage

Meneja undelezaji Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Mhandisi Danford Semwenda amesema kuwa ni kazi ngumu kuwadhibiti mawakala wa uuzaji wa saruji hiyo hivyo wanaomba ushirikiano kutoka serikali ili kudhibiti hali hiyo.

Naye Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Camel, Ghalib Hassan Ghalib  alisema kutokuwapo kwa umeme wa uhakika nao umekuwa kikwazo kwa kiwanda hicho kufikia malengo ya kuzalisha tani 600 kwa siku na hivyo kuzalisha tani 400.

Video: Manchester United yachakazwa bao 3- 0 na Spurs
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 28, 2018