Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally Mbwana ametangaza kwa umma kuwa sikukuu ya Eid El- Adh’haa itakuwa tarehe 31 Julai 2020, siku ya ijumaa.

Maadhimisho ya sikukuu hiyo kitaifa yatafanyika mkoa wa Dar es salaam, ambapo swala ya Eid kitaifa itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi na Baraza la Eid litafanyika hapo hapo mara tu baada ya swala hiyo.

Taarifa iliyotolea na katibu Mkuu, Nuhu Jabirinaeleza kuwa kwaniaba ya Baraza kuu la waislamu wa Tanzania, Mufti anawatakia waislamu na wananchi wote sikukuu njema na anawaomba kusherehekea kwa salama na amani huku wakichukua tahahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Setien, Messi wazika tofauti zao, wageukia UEFA
JPM aagiza Mbuyu wa Nyerere Dodoma kufanywa Makumbusho