Ili kuhakikisha Tasnia ya Habari inakuwa na sheria rafiki na zinazotekelezeka, Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa amesema atashirikiana na Wabunge wenzake kuzungumzia baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya Habari ya mwaka 2016, vinavyokandamiza uhuru wa Habari nchini.

Akizungumza na Uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), jijini Dodoma Silaa amesema hakuna asiyefahamu kuwa Dunia kwasasa imebadilika na kwamba haiwezekani kuendelea kubaki nyuma hivyo mabadiliko ni wajibu.

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa (kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.

Awali, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, Deodatus Balile alimweleza Jerry Silaa kuwa sheria ya habari ya mwaka 2016 imeweka mazingira ya hofu kwa mwandishi wa habari, na kwamba, ndani ya sheria hiyo kuna vipengele vinavyoua tasnia ya habari.

Naye, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), tawi la Tanzania, James Marenga alimweleza Mbunge huyo kuwa, kama mawakili wanatengeneza taratibu zao na kuzifanya kuwa rejea katika kazi zao, ni vyema pia Wanahabari wakafuata mfano huo.

Umakini wakati wa maongezi juu ya Sheria ya Habari na Mbunge wa ukonga.

‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza cord of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongozi, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd, Jessy Kwayu alisema, sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katika mazingira yasiyo rafik na kwamba vipengele 19 vya sheria hiyo vilijaribiwa kwenye sheria za nchi, na kuonekana kutoingia katika mizani ya kisheria akiungana na Rose Reuben aliyesema kwa mazingira ya sasa, Waandishi wawapo huru kiutendaji.

Mauaji ya Mwandishi Kenya yalipangwa: Waziri
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 9, 2022Â