Rais wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi ametangaza tarehe maalum ya kuiuza klabu hiyo kwa wafanyabiashara kutoka mashariki ya mbali.

Berlusconi aliweka hadharani siku ya kufanya biashara ya kuiuza klabu hiyo aliyodumu nayo kwa zaidi ya miongo miwili, alipohojiwa katika kipindi cha televisheni kiitwacho Matrix.

Alisema mpango wa kuiuza AC Milan umekaribia na atafanya hivyo kutokana na dhamira ambayo aliiweka moyoni mwake kwa miaka mingi iliyopita.

“Nitafanya biashara ya kuiuza klabu hii itakapofika Disemba 13, kwa nimeshafanikisha asilimia kubwa ya hatua ya mauzo,” alisema Berlusconi.

“Endapo itakua kinyume na matarajio hayo, nitakua radhi kubaki na umiliki wa klabu yangu, kutokana na hitaji la kutaka kuiona inafikia hatua kubwa zaidi ya ilivyo sasa, lakini nina uhakika mambo yatakua mazuri.”

Hata hivyo Berlusconi ametoa sababu za kutaka kuiuza klabu hiyo kwa kusema kuna mambo mengi yaliyomsukuma kufanya maamuzi hayo, likiwepo suala la mtaji mkubwa wa kuiendesha AC Milan.

“Milan inahitaji mtaji. Ni maamuzi magumu kwangu, lakini sina namna ya kufanya zaidi ya kuiingiza sokoni ili iendeleee kupata manufaa zaidi duniani, Ni jambo la kawaida kwa wafanyabiashara kufikia hatua hii ya kuuza ama kununua, hivyo nimeridhia kufanya jambo hili. Nilitamani kubadili mfumo ili tufanane na Real Madrid ama FC Barcelona kwa kuuza sehemu ya hisa kwa wanachama, lakini bado nimegundia mpango huo hauwezi kuleta mabadiliko ya kibiashara.” Alisema Berlusconi

Video: Siri nzito kikao cha JPM, Lukuvi, Serikali yashtuka...
Jose Mourinho: Messi Hang'oki Camp Nou