Rais wa klabu ya AC Milan ya nchini Italia, Silvio Berlusconi amekubali kufanya mazungumzo upya kuhusu ofa ya iliyowasilishwa na wawekezaji kutoka nchini China, ambao wapo tayari kuwekeza klabuni hapo kwa kusaidiana na uongozi uliopo.

Wawekezaji hao kutoka kwenye kampuni ya TMW, waliwahi kuwasilisha ofa ya Euro Milion 550, kwa kuamini ingekua rahisi kwao kufanikisha lengo wanalo likusudia lakini rais wa AC Milan aliikataa.

Hata hivyo uongozi wa kampuni hiyo uliamini kiasi hicho kingetosha kutokana na madeni yanayoiandama klabu ya AC Milan kwa sasa, ambayo walikua tayari kuyalipa kama wangekubaliwa.

Kwa mara ya pili Berlusconi, aliwakatalia wawekezaji hao ofa nyingine ambayo ilifikia kiasi cha Euro million 750, kwa kusisitiza haitoshi kuwekezwa kwenye klabu kubwa kama AC Milan ambayo imewahi kutwaa taji la barani Ulaya mara saba.

Kutokana na msimamo huo, wawekezaji hao kutoka China wameafiki kukutana na Berlusconi kwa mara ya tatu, ili kuanza upya mazungumzo ambayo yanatarajiwa kuzaa matunda kwa pesa nyingi kuwekezwa.

Kama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, klabu ya AC Milan inatabiriwa kurejea katika hali yake ya kiushindani kama ilivyokua mwanzoni mwa miaka ya 2000, na imebainika huenda wachezaji wenye tahamani kubwa duniani wakaanza kusajiliwa huko San Siro.

Mario Gotze Kucheza Soka Nchini England Msimu Ujao?
Chelsea Wajipanga Kwa Vita Ya Kumuwania Alvaro Morata

Comments

comments