Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Simba ameonekana katikati ya jiji la Nairobi nchini Kenya akijiachia katikati ya barabara lenye foleni kali kabla ya kumjeruhi mzee mmoja mwenye umri wa miaka 63, mapema leo asubuhi.

Msemaji wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS), Paul Udoto amewaambia waandishi wa habari kuwa Simba huyo ametoroka kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Nairobi (Nairobi National Park) na kuingia kwenye jiji hilo lenye takribani watu milioni 3.

Udoto alisema kuwa Simba huyo amemjeruhi mzee huyo baada ya kuchukizwa na honi pamoja na kelele alizokuwa akipigiwa, lakini hakuathiri sana. Kwa mujibu wa Udoto mzee huyo alipelekwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta akapewa huduma ya kwanza na baadae kukimbizwa hospitalini.

“Watu walikuwa pale wakipiga honi na kujipiga ‘selfies’ na Simba akapata mshtuko na kukasirishwa,” alisema Udoto.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha Simba huyo akiwa katikati barabara ya Mombasa yenye njia nne, huku watu wakipiga ‘mapicha’ na honi.

Hata hivyo, Askari wa Hifadhi ya Taifa la Kenya walimsindikiza Simba huyo hadi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Nairobi na kuhakikisha anaingia ndani zaidi.

Simba 2

Ulinzi na msako unaendelea kujiridhisha kama hakuna Simba wengine waliotoroka na kuingia ndani ya jiji hilo. Hii sio mara ya kwanza kutokea tukio kama hilo jijini humo.

Msukuma amsema Kikwete kwa Majaliwa
Wachezaji Wa Simba Wajazwa Fedha Kwa Ushindi Mfululizo