Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wameanika hadharani majina ya wachezaji wa TP Mazembe watakaokuja nchini kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa Jumapili (Septamba 19).

Simba SC wanatarajiwa kuutumia mchezo huo kama sehemu ya kusherehesha Tamasha la Simba (Simba Day), litakalofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC wameanika majina ya wachezaji wa TP Mazembe kupitia kurasa zao za mitandao ya Kijamii kwa kuandika; “Kikosi cha wachezaji 23 wa TP Mazembe ambacho kitatua nchini jumamosi kuja kuwakabili mabingwa wa Tanzania na timu inayowakilisha nchi vizuri kimataifa Simba SC katika kilele cha Wiki ya Simba (Simba Day 2021).”

Lyanga kufanyiwa uchunguzi Azam FC
Young Africans yakanusha taarifa za Kocha Nabi