Klabu ya Simba ambao ni vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kupata nguvu mpya kwenye eneo lake la ulinzi kwa kuanza kuwatumia mabeki wake Shomari Kapombe na Asante Kwas

Simba SC huenda ikaanza kuwatumia nyota hao leo kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar itakapocheza na timu ya Mwenge.

Kapombe na Kwasi jana wamefanya mazoezi ya mwisho hivyo kocha wa timu hiyo, Juma Masoud, anaweza kuamua kuwaanzisha.

Aidha, Kapombe alikuwa majeruhi kwa muda mrefu tangu asajiliwe kutoka Azam FC hivyo kurejea kwake katika kikosi hicho, kutaimarisha safu ya ulinzi.

Hata hivyo, Klabu hiyo ya Msimbazi itaanza rasmi michuano ya Mapinduzi Cup leo dhidi ya Mwenge. mchezo huo utapigwa saa 10:30 jioni kwenye uwanja wa Aman.

 

TRA: Hatuhitaji kulumbana na Askofu Kakobe
Lissu: Dereva wangu ameniendesha miaka 15, nilitendewa tukio nikiwa nae na nitahojiwa nikiwa nae