Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo Jumatatu (Septambe 27) kitaelekea mjini Musoma mkoani Mara, tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.

Simba SC ambao ni Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu wataondoka Mwanza, baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo jijini humo wakitokea Dar es salaam, ambako walikuwa na mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao wa jadi Young Africans.

Simba SC itaanza kutetea taji la Tanzania Bara kwa kucheza dhidi ya Biashara United Mara kesho Jumanne (Septamba 28), katika Uwanja wa Karume mjini Musoma.

Simba SC itacheza mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Coastal Union yatamba kushinda nyumbani
Serikali yatoa maagizo maegesho ya Mv Mwanza