Wekundu Wa Msimbazi Simba kesho watajitupa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanza harakati ya kupambana kimataifa kwa kucheza na klabu ya Gendamarie ya nchini Djibout, katia michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Simba wataingia uwanjani hiyo kesho huku wakiwa na muenendo mzuri katika ligi kuu ya soka Tanzania bara, hali ambayo inaaminiwa na mashabiki na wanachama wao kuwa, huenda ikawa chachu ya wachezaji wao kuendeleza furaha.

Simba wanarejea katika michuano ya kimataifa baada ya miaka sita kupita, huku wakiwa hawawafahamu vyema wapinznai wao kutoka nchini Djibout, ambao itakua mara yao ya kwanza kucheza katika ardhi ya Tanzania.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amesema kutokana na uzito wa mchezo huo wa kesho, wanaamini mashabiki wa soka nchini hususan wa klabu hiyo watajitokeza kwa wingi katika uwanja wa taifa, kwa lengo la kwenda kuipa ushirikino timu yao, ambayo ina hamu ya kuwapa ladha ya ushindi.

Totenham Hotspurs yaishushia kipigo Arsenal
Young Afrcans waanza kwa ushindi kiduchu

Comments

comments