Simba imepata ushindi wa goli 1 bila dhidi ya Ndanda FC, goli hilo limefungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 44.

Mpaka kufikia sasa Simba wanahitaji point 1 ili kuibuka washindi wa Vodacom Premier League (VPL) msimu huu wa mwaka 2017/2018, na wamebakiwa na mechi tatu kucheza dhidi ya Singida United, Kagera Sugar na Majimaji FC.

Hata hivyo baada ya mechi saba za raundi ya 27 kukamilika leo hadi sasa ni wazi kuwa Simba wanakaribia ubingwa kwa kishindo kikubwa kwani ndio timu pekee hadi sasa kuvunja rekodi ya kucheza mechi zote msimu huu bila kufungwa.

Mbali na mechi ya Simba na Ndanda FC mechi nyingine zilizocheza leo ni Stand United dhidi ya Azam Fc ambapo Stand United imeibuka na ushindi wa bao 2 kwa bao 1, huku Kagera Sugar imetoa suluhu na Mbeya City alikadhalika Majimaji FC na Mtibwa Sugar.

 

Waziri apigwa risasi kwenye mkutano wa kampeni
Waliojihami kwa silaha wavamia kijiji na kuua makumi