Baada ya Azam FC kufanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuivurumisha Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliotimua nyasi mwishoni mwa mwaka jana (2015) kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi tena Ijumaa hii kwa mchezo mmoja kuendelea.

Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwala unatarajia kuwakutanisha wenyeji wa uwanja huo, Ndanda FC, wanakuchele dhidi ya mnyana, Simba SC, mchezo utakaopigwa majira ya saa kumi jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Simba inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kwenda sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mwadui FC.

Hata hivyo wekundu hao wanaonekana kuwa na mwenendo wa kusuasua baada ya kutopata ushindi kwenye michezo miwili mfululizo.

Simba ipo kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi 24, baada ya kucheza michezo 12 na kufanikiwa kushinda michezo 7 pekee.

Danny Welbeck Atuma Salamu Za Mwaka 2016 Afrika
Louis van Gaal Aendelea Kuweweseka Man Utd