Mjadala wa timu za Simba na Yanga kwenda kucheza kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi ambao ni uwanja wa nyumbani wa Azam FC umefikia mwisho baada ya Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kutoa msimamo wake juu ya jambo hilo.

Kidao amesema uwanja wa Azam Complex umechelewa kupewa haki yake ya Simba na Yanga kucheza pale huku akihoji kwamba kama mechi za CAF zinachezwa Chamazi ni kwanini Simba na Yanga nao wasitumie uwanja huo katika mechi wanazokuwa ugenini wakicheza na Azam?

”Azam Complex ni uwanja ambao tayari ulisharuhusiwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kuchezewa mechi za kimataifa leo hii ukiwa unauliza kwa nini mechi za Simba na Yanga zipelekwe Chamazi ni jambo la kushangaza” alisema Wilfred Kidao.

Katibu huyo wa TFF ameongeza uwanja wa Azam Complex umechelewa kupewa haki yake lakini kikubwa kuliko yote ni kwamba watu waliofanya uwekezaji mkubwa namna ile unapowanyima fursa ya kuutumia uwanja wao kwa mechi zote unakuwa hauwatendei haki.

Akitoa takwimu ya mashabiki wanaoingia katika uwanja wa Taifa unaoingiza mashabiki 60,000 wakati wa mechi za Yanga na Simba Kidao amesema mechi ijayo ya Simba na Yanga itachezwa uwanja wa Uhuru, uwanja ambao unaingiza mashabiki wasiozidi 25,000 lakini itachezwa na kikubwa ni kuhakikisha usalama unakuwepo tiketi zikiisha hakuna mtu ataeingia uwanjani.

Kitendo cha mechi za Azam dhidi ya Simba na Yanga kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa kinazinufaisha timu mbili za Yanga na Simba kwa sababu zinakuwa na mechi nyingi za nyumbani ukilinganisha na Azam.

 

Chebukati ateua tume mpya ya uchaguzi Kenya
Dawa za kuongeza nguvu za kiume zapigwa marufuku