Baraza la Vyama Vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati *CEFACA* limepanga makundi ya michuano ya klabu Bingwa kwa Wanawake iliopangwa kuunguruma nchini Kenya kuanzia Julai 17 hadi Agosti Mosi.

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba Queens ambao wataiwakilisha nchi kwenye Michuano huyo wamepangwa kundi A lenye timu za Doves ya Uganda na PVP ya Burundi.

Simba Queens italazimika kushinda na kuwa Bingwa wa Michuano hiyo,  ili kupata tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Barani Afrika kwa wanawake msimu wa 2021/22.

Kundi B lina timu za Commercial Bank of Ethiopia (Ethiopia), Uri Joint stars (South Sudan) na New Generation Queens (Zanzibar).

Kundi C kuna timu za Scandinavian FC (Rwanda), FAD club (Djibout) na Vihiga Queens (Kenya)

Bingwa wa Michuano ya Wanawake kila Kanda Barani Afrika atakata tiketi ya kushirki moja kwa moja Ligi ya Mabingwa.

Dkt. Ndumbaro: Mabwawa yaanze kuchimbwa mara moja
Waziri Mkumbo azindua Bodi ya wakurugenzi TBS