Bao lililofungwa na Kiungo kutoka nchini Uganda Thadeo Lwanga dakika ya 80, limetosha kuipa ubingwa wa Kombe la Shirikisho *ASFC* Simba SC kwa mara ya pili mfululizo.

Simba SC ilikua na kibarua kizito dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Fainali ulipigwa mjini Kigoma, Uwanja wa Lake Tanganyika, leo Jumapili (Julai 25).

Lwanga alifunga bao la ushindi kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na kiungo wa kimataifa kutoka Msumbiji, Jose Luis Miquissone.

Young Africans ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 na ushei baada ya kiungo kutoka DR Congo, Tonombe Mukoko kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.

Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 26, 2021
Lazima mahabusu wapimwe -Prof. Makubi