Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamefanikiwa kunyakua taji la Mapinduzi Cup mara baada ya kuichapa Azam FC bao 1-0.

Mchezo huo uliokuwa na upinzani mkubwa uliudhuliwa na Rais wa Serikali yaa MapinduI Zanzibar Hussein Ali Mwinyi ambaye alikua Mgeni Rasmi.

Bao pekee la Simba SC liliwekwa kimyani na Meddie Kagere ambaye alipachika kwa mkwaju wa penati mara baada ya Sakho kuchezewa faulu ndani ya boksi na Mlinda Lango wa Azam FC Mathias Kigonya.

Mchezo huo ambao ulikuwa na hisia kwa mashabiki waliohudhuria Uwanja wa Amani ulikuwa ma mvuto wa aina yake kufuatia kila timu kuonesha uwezo wa kupambana.

Simba SC yalamba tuzo zote Mapinduzi CUP 2022
Kenyatta aonesha wazi mrengo wake kuelekea uchaguzi mkuu Kenya.