Mabingwa wa Soka na Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Simba SC leo Ijumaa (Februari 05) wameingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kutumia neno ‘VISIT TANZANIA’.

Simba SC wamesaini dili hilo leo mchana mjini Dodoma katika hafla maalum ilihudhuriwa na waandishi wa habari, pamoja na Waziri mwenye dhamana ya utalii Damas Ndumbaro.

Dili hilo linaifanya Simba SC kubeba jina la ‘VISIT TANZANIA’ ambalo limeambatana na picha ya Mlima Kilimanjaro kwenye jezi ambazo zitazitumia katika michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika itakayoanza Februari 12.

Simba SC imefikia hatua hiyo kufuatia sheria na kanuni za Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ linaloendesha michuano ya Ligi ya Mabingwa kuzinyima nafasi klabu zinazodhaminiwa na makapuni ya kubashiri matokeo ‘BETTING’, kutumia jezi zenye nembo ya makampuni hayo, pindi zinapokua kwenye mchakato wa kusaka alama tatu muhimu.

Simba SC imepangwa kundi A pamoja na mabingwa wa kihistoria wa Barani Afrika Al-Ahly SC ya Misri, Al-Merrikh SC ya Sudan na bingwa mara moja pamoja na kuwa mshindi wa pili mara mbili, AS Vita Club.

Simba SC itanza kusaka taji la Afrika kwenye hatua ya makundi msimu huu kwa kucheza dhidi ya AS Vita Club, mjini Kinshasa February 12.

Taasisi na vyuo vya afya vyatakiwa kushirikiana kuboresha tiba asili
Wanaume wanaongoza kufa kwa UKIMWI