Mabingwa wa Tanzania Bara na Wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Simba SC, kesho wataanza mazoezi rasmi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi Ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Kikosi cha Simba SC kilirejea jana Jumatatu (Oktoba 18) kikitokea Gaborone, Botswana ambako walicheza dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumapili (Oktoba 17), na leo Jumanne (Oktoba 19) wachezaji walikuwa mapunziko.

Simba SC inajiandaa na mchezo wa mkondo wa pili, huku ikikumbuka ushindi wa mabao 2-0, mjini Gaborone.

Mabao wa Simba SC katika mchezo huo yalifungwa na Nahodha na Mshambuliaji John Bocco dakika ya 02 na 05.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Jumapili (Oktoba 24), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Sikutegemea "Essence":Wizkid
Young Africans yafika kileleni