Kikosi c ha Mabingwa wa Soka Tanzanai Bara Simba SC kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea Mkoni Morogoro Kesho Alhamis (Januari 20) au Keshokutwa Ijumaa (Januari 21), tayari kwa mchezo wa mzunguuko wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumamosi (Januari 22).

Simba SC ilirejea jana Jumatano jijini Dar es salaam ikitokea Mbeya ilipokua inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu mzunguuko wa 12 dhidi ya Mbeya City iliyochomoza na ushindi wa bao 1-0, siku ya Jumatatu (Januari 17).

Meneja wa habari na mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema kikosi chao baada ya kurejea Dar es salaam kilipewa mapumziko, na leo Jumatano (Januari 19) majira ya asubihi kimerejea kambini, kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Amesema safari maandalizi ya safari ya kuelekea Morogoro yanaendelea vizuri na wamepata uhakika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utachezwa Manungu Complex, hivyo timu yao itakapofika mjini Morogoro itapumzika kabla ya kuendelea na Safari ya kuelekea Wilayani Mvomero yalipo maskani ya Mtibwa Sugar.

“Tumerejea jana kutoka mbeya na jana hiyo hiyo wachezaji walipewa ruhusa ya kwenda kusaliamia familia, leo majira ya saa mbili asubuhi kikosi kimejikusanya kambini maeneo ya Bunju, na kimeanza mazoezi kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar,”

“Tutaondoka Dar es salaam kwenda Morogoro kati ya tarehe 20 au 21 kwa sababu mchezo utachezwa Manungu, na huko mazingira sio rafiki sana, kwa hiyo tutalala Morogoro, na siku ya mchezo tutaelekea Manungu.” Amesema Ahmed Ally

Simba SC inaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 24, ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 32.

Mbivu, mbichi Uspika CCM
Ahmed Ally: Lwanga amenusurika Simba SC