Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC watakabidhiwa Kombe la Ubingwa Julai 18, baada ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Taarifa iliotolewa leo Jumanne (Julai 13) asubuhi na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) iimethibitisha kuwa Mabingwa hao mara nne mfululizo watakabidhiwa Kombe la ubingwa siku hiyo.

Simba SC ilijitangazia Ubingwa Juzi Jumapili (Julai 11), baada ya kuibamiza Coastal Union mabao 2-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Klabu hiyo ya Msimbazi-Kariakoo jijini Dar es salaam imefikisha alama 79, baada ya kucheza michezo 32 huku ikibakiza michezo miwili.

Young Africans inayoshika nafasi ya pili ina alama 70, baada ya kucheza michezo 32, huku ikibakiza michezo miwili.

Ni dhahir Young Africans haiwezi kufikia alamab 79 hata ikishinda michezo yake iliyobaki.

Mwigulu: Young Africans itakuwa imara 2021-22
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 13, 2021