Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Julai Mosi), kikitokea mjini Songea mkoani Ruvuma kilipokua na kazi ya kupambana kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2021/22.

Simba SC ilicheza na Mbeya Kwanza FC katika Uwanja wa Majimaji juzi Jumatano (Juni 29), na kuambulia sare ya bila kufungana ambayo bado iliendelea kuwaweka nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu, ikitaguliwa na Mabingwa Young Africans.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amethibitisha taarifa za kurejea kwa kikosi cha klabu hiyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ahmed Ally ameandika: Kikosi chetu kinarejea leo Dar Es Salaam kutokea Songea

Wachezaji wanaenda mapumziko kula maisha na familia zao

Tutawapa taarifa ni lini tutarejea tena kuanza maandalizi ya msimu ujao na wapi tutafanyia maandalizi yetu

Kuhusu usajili unaendelea ndani kwa ndani muda ukifika tutaweka hadharani majina yote

Wakati huu wa mapumziko nanyi mashabiki wetu pumzikeni mkusanye nguvu za Simba Day na msimu ujao

Ni muhimu kutumia mapumziko haya kumwagilia moyo

Ngara yapata hati safi, RC awataka Madiwani kusimamia mapato
Cleophace Mkandala ameaga rasmi Dodoma Jiji FC