Uongozi wa Simba SC umefanya mazungumzo na Nyota watatu wapya wa Kimataifa kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao kuelekea Dirisha Dogo la Usajili litakalofunguliwa mwezi ujao.

Hadi sasa Simba SC imeshafanya mazungumzo na Winga kutoka nchini Msumbiji, Kiungo mkabaji raia wa Senegal na Mshambuliaji raia wa Ghana.

Taarifa za ndani zinadai kuwa, ongezeko la Nyota hao linatokana na baadhi ya wachezaji waliosajiliwa kwenye Dirisha Kubwa kama Victor Akpan na Nelson Okwa, ambao wana uraia wa Nigeria na Mohamed Ouattara raia wa Ivory Coast kushindwa kuonyesha cheche, licha ya kusajiliwa kwa fedha nyingi mwanzoni mwa msimu huu.

Chanzo cha Habari kutoka Simba SC kimeeleza kuwa , Uongozi umelazimika kufanya Usajili huo mapema kwa kuwapata Nyota watatu katika nafasi ya Mshambuliaji, Kiungo Mkabaji na Winga ili kuwahi Michuano ya Kimataifa, ambapo Simba SC imetinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

“Kuna uwezekano mkubwa wa Dirisha Dogo la Usajili kupata saini ya Luis Muquissone raia wa Msumbiji, ila pia kuna mchezaji kutoka Ghana na Winga mpya raia wa Senegal ambao kwa pamoja wameshamalizana na Uongozi,” kimeeleza chanzo hicho

Simba SC ina kiu ya kurejesha Ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2022/23, sambamba na kuvuka hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Harry Kane kuivaa Marekani leo
Aziz Ki aongeza mzuka Young Africans