Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema klabu hiyo ya Msimbazi itakuwa sehemu ya klabu zitakazoshiriki Michuano ya AFRICAN SUPER CUP.

Try Again amethibitisha ushiriki wa Simba SC kwenye michuano hiyo alipohutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Klabu hiyo, unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam, leo Jumapili (Januari 29).

Mbali na hilo, Try Again amezungumzia masuala mengine yanahohusu Simba SC, sambamba na kuwashukuru Mashabiki na Wanachama kwa kuvumilia Panda Shuka za klabu yao.

“Nawashukuru wanachama na mashabiki wetu, tumepitia kipindi kigumu lakini mmeendelea kuwa nasi. Kwa niaba ya bodi tunawashukuru sana.”

“Sasa tupo namba 10 Afrika kwa ubora wa vilabu. Tupo katika mapambano ya ligi, ligi ni ngumu lakini sisi viongozi tumejipanga timu yetu kupambana na mwaka huu kushinda ubingwa.”

“Haya mafanikio hayakuja kwa bahati mbaya, sina budi kumshukuru Ndg. @moodewji kwa upendo wake, ametumia pesa zake, muda wake, nguvu yake kuhakikisha tunayafikia mafanikio haya. Tuendelee kumtia moyo, amefanya kazi kubwa.”

“Hivi karibuni tutapokea ujumbe kutoka FIFA na CAF kuja kugagua kama mnavyojua Simba ndio timu pekee kutoka ukanda wa CECAFA ambayo itashiriki Super Cup.”

“Sina budi kumshukuru CEO aliyepita, amefanya kazi kubwa. Nachukua nafasi hii kumshukuru na namuombea dua katika changamoto yake mpya.”

“Sasa kila mchezaji mkubwa Afrika anataka kuja kucheza Simba. Nawahakikishie Simba ile ya furaha inarudi, hatutakuwa wanyonge tena, Simba hii ni ya kimataifa.”

“Nimepokea mwaliko mwingine kwenda kwenye semina ya FIFA kule Morocco. Hii ni kwa ajili ya Simba. Katika watu watatu Afrika mimi ni mmoja wao kwenda kuwawakilisha.” amesema Try Again

Manzoki avunja ukimya Dar es salaam
Imani Kajula aweka wazi Simba SC inakoelekea