Klabu ya Simba huenda ikanusa ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, endapo itafanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons wanaokutana nao baadae hii leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba wanaoongoza msimamo wa ligi kuu, kwa sasa wana alama 55, na kama watafanikiwa kupata alama tatu dhidi ya maafande hao wa Jeshi La Magereza watakua wanafikisha alama 58 na kuwaacha wapinzani wao Young Africans kwa alama 11.

Young Africans ambao watakua na michezo miwili mkononi dhidi ya, baada ya mpambano wa leo kati ya Simba na Tanzania Prisons kumalizika uwanja wa Taifa, wapo katika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 47.

Kimahesabu Simba watakua wamesaliwa na michezo sita, baada ya mchezo wao wa leo, na Young Africans wanaendelea kusaliwa na michezo minane kufikia ukingoni mwa ligi kuu msimu huu wa 2017/18.

Kama Simba leo watashinda watakua wakihitaji alama nyingine tano ili kutimiza ndoto za kutwaa taji la ligi kuu msimu huu, na kumaliza ukame wa miaka zaidi ya minne ambayo ilishuhudia Wanamsimbazi hao wakitoka kapa.

Israel kuwaachia wafungwa 200 wa Kiafrika
Mshairi atupwa jela miaka 3 kwa kuhamasisha umoja

Comments

comments