Kalamu ya @swalehmawele

Mechi ngumu kwa upande wa timu zote mbili, Polisi Tanzania ipo katika nyakati nzuri kwa sasa wakipata ushindi wa asilimia mia moja katika ligi, wamepata ushindi katika mechi tatu za ligi.

Simba imepoteza mechi ya mwisho na imetoka katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika, nini wachezaji wanawaza muda huu? mchezo wa mpira wa miguu unachezwa zaidi kichwani na miguuni inakuwa ni uwasilishwaji wake tu.

Wanakwenda kucheza na Polisi Tanzania ambayo kila kitu kwao kinaonekana kuwa sawa, wanafunga magoli na wanazuia vizuri, clean sheets mbili, wamefunga magoli matano na wameruhusu goli moja tu kwenye ligi.

Bahati mbaya kwa Polisi Tanzania wanakwenda kucheza na Simba ambayo imefanya mabadiliko katika benchi la ufundi, kama wachezaji wataingia kwa kuitaka mechi hii na kuzitetea nafasi zao ndani ya timu wanaweza kuwa na mechi ngumu zaidi hasa ukitazama wanacheza katika dimba la Mkapa.

Kama Polisi Tanzania watafanikiwa kuidhibiti Simba katika kipindi cha kwanza kwa wao kutangulia au kuwa na mzani sawa wa magoli wanaweza kuiweka Simba katika nyakati ngumu sana.

Wanaweza kuifanya Simba ipaniki zaidi na kama wao wataongeza umakini wanaweza kuwa na wakati mzuri wa kuondoka na alama, hii yote ni kwa sababu hali haiko sawa kwa Simba na kila zuri limeegemea upande wa Polisi Tanzania.

China yatangaza ‘Lockdown’
Fei Toto: Sitachoka kuibeba Young Africans