Uongozi wa klabu ya Simba SC umewashukuru watanzania waliojitokeza kuwapokea mjini Khartoum walipokwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya makundi.

Kikosi cha Simba SC kiliwasili mjini Khartoum leo alfajiri (saa tisa usiku) kikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia kilipobadilisha ndege, baada ya kuondoka jijini Dar es salaam, majira ya jana jioni.

Simba SC imetoa shukurani hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii huku ikiweka picha ya mapokezi walioyapata kutoka kwa watanzania waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, Sudan kuwapokea.

Simba SC wameandika: “Popote tuendapo tunapokelewa kama tupo nyumbani. Asanteni Watanzania wenzetu mliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, Sudan kutupokea wawakilishi wa nchi kwenye #TotalCAFCL #NguvuMoja”

Leo Alhamis kikosi cha kikosi cha Simba SC kitaanza mazoezi kikiwa mjini Khartoum, na kitafanya hivyo kesho kwenye uwanja Al Merrikh utakaotumika keshokutwa Jumamosi (Machi 06).

Simba SC inaongo za msimamo wa ‘KUNDI A’ kwa kumiliki alama sita, baada ya kuzifunga AS Vita Club ya DR Congo na Al Ahly ya MIsri.

Mawaziri wapya wala kiapo
Kesi ya mauaji ya Khashoggi yaanza tena