Baada ya kufanya mazoezi ya nguvu juma lililopita, kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba juma hili kimeanza mazoezi ya mbinu.

Kocha Sven Vandenbroeck akishirikiana na benchi lake la ufundi, kuanzia jana Jumatatu alianza kuwafanyisha wachezaji wake mazoezi machache ya viungo, na baada ya hapo wakafanya mazoezi ya kuchezea zaidi mpira.

Aina ya mazoezi hayo yalikuwa ni jinsi ambavyo timu yao itakuwa inazuia kwa maana ya kukaba timu pinzani, ambazo watakutana nazo kuanzia Juni 14 wakianza dhidi ya Ruvu Shooting.

Mazoezi mengine ambayo yameanza kuonekana kwenye kikosi cha mabingwa hao ni jinsi ambavyo watashambulia kwa aina tofauti, kwa maana ya kupitia pembeni na kati kati ya uwanja.

Mazoezi mengine ni kupiga mashuti ya mbali, pasi ndefu na fupi kuanzia nyuma mpaka kufika langoni mwa timu pinzani, kufungua nafasi (Open Spaces), kisha mazoezi ya kunyoosha viungo.

Aristica Cioaba kuanza kazi rasmi
Ripoti kifo cha George Floyd zatofautiana, Serikali yadai ‘alikuwa anaumwa’, wataalamu waja na yao