Uongozi wa klabu ya Simba, umeitaka radhi serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kufuatia uharibufu mkubwa uliofanywa na mashabiki wa klabu hiyo kwa kung’oa viti vya uwanja wa taifa wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara aliwasilisha ujumbe wa viongozi wake wa kuomba radhi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema hii leo, makao makuu ya klabu hiyo yaliopo mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam.

“Nichukue fursa hii kuiomba msamaha serikali juu ya vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Simba na kusababisha hasara kubwa ambayo sisi kama klabu itatubidi tulipe kwani hakuna jinsi na tunalaani vitendo hivyo”.

Mashabiki wa klabu ya Simba walifikia hatua ya kung’oa viti vya uwanja wa taifa baada ya kuchukizwa na maamuzi ya mwamuzi Martin Saanya ya kulikubali bao la mshambuliaji wa Young Africans Amissi Tambwe, ambaye anadaiwa aliushika mpira kabla ya kuukwamisha wavuni.

Vurugu zilizofanywa na mashabiki wa simba zimepelekea Serikali kuufunga uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana na kuziambia klabu zinazoutumia uwanja huo (Simba, Yanga na African Lyon) vitafute sehemu nyingine kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani

 

Santi Cazorla: Bado Ninaipenda Arsenal FC
Waziri Nchemba aagiza msako wa walimu wanaoonekana kwenye video wakimshambulia mwanafunzi