Ndugu wana habari, klabu ya Simba inayo furaha kuwatangazia umma kupitia kwenu kwamba, itacheza mechi nyingine ya kirafiki ya kimataifa siku ya Jumapili inayokuja ya tarehe 14-8-2016 kuanzia saa kumi alasiri kwenye uwanja wa Taifa ulipo jijini Dar es salaam.

Safari hii timu yetu imeialika klabu ya inayomilikiwa na Mamlaka ya mapato nchini Uganda URA.

Benchi la ufundi litaitumia mechi hiyo kama sehemu ya mwisho ya maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza baadae mwezi huu.

Viingilio kwenye mchezo huo ni Shilingi elfu ishirini kwa VIP A, elfu kumi na tano kwa VIP B na C na shilingi elfu tano kwa mzunguko.

Nitumie fursa hii pia kuendelea kuwahabarisha kuhusu usajili wa mshambuliaji wetu wa kimataifa wa Burundi Laudert Mavugo kuwa ni mchezaji atakaetumika kwenye msimu huu wa ligi kuu katika klabu yetu na kama yapo makubaliano yoyote baina yetu na klabu za nchini kwao ni mambo ya ndani ya kiofisi.

Pia niviase baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viwe na umakini mkubwa vinapotoa habari ili kutowachanga wanachama na washabiki wetu.

Ni vizuri vikapata taarifa za uhakika kwanza kutoka kwetu, kuliko kujiandikia ili tu kujifurahisha.

Mwisho niwaombe na kuwasisitiza wanachama na washabiki wetu, wasiyumbishwe na ‘POROJO’ za wasiotutakia mema hiki ndio kipindi muhimu cha kuendeleza umoja wetu ambao hauthaminishwi na kitu chochote kile.

Imetolewa na

Haji S Manara

Mkuu Wa Habari

Simba Sc

Simba Nguvu Moja

FIFA Yatoa Orodha Ya Viwango, Tanzania Yaporomoka Tena
Young Africans Wasubiri Maamuzi Ya FIFA