Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, umetangaza hadharani mipango na mikakati kuelekea msimu mpya wa 2021/22, ambapo watakua na kibarua kizito cha kutetea ubingwa kwa mara ya tano mfululizo.

Msimu wa 2020/21 Simba SC ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara mara nne mfululizo, huku wakiishia Hatua ya Robo Fainali katika michuano ya Ligi ya Mbaingwa Barani Afrika, baada ya kufungwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini mabao 4-3.

Mwenyekiti wa Simba SC Multaza Mangumgu amesema dhamira yao kubwa kuelekea msimu ujao ni kuendeleza ufalme wa soka katika ardhi ya Tanzania Bara, huku Barani Afrika wakijipanga kufika hatua ya Nusu Fainali na ikiwezekana Fainali.

Mangungu amesema maandalizi ya kikosi chao yanawapa picha ya kuendeleza ubabe katika Ligi ya Tanzania Bara huku Benchi lao la Ufundi linaloongozwa na Kocha Didier Gomes lipo imara na makini.

“Tuna kikosi chenye wachezaji wazuri ambao wapo kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu mpya. Jambo kubwa ni kuona kwamba yale mataji ambayo tulitwaa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara tunalichukua.

“Kwa sasa tunachokifanya ni maandalizi kwani hakuna kinachowezekana kutokea kama hakutakuwa na mipango. Benchi la ufundi tulilonalo ni la kazi mpaka vifaa pia tunavyo, hivyo mashabiki waendelee kuwa bega kwa bega na sisi.” amesema Mangungu

Kwa sasa kikosi cha Simba SC kipo Arusha kwa ajili ya awamu ya pili ya kambi ya maandalizi ya msimu wa 2021/22, baada kuamliza awamu ya kwanza nchini Morocco.

Bongo Zozo ampongeza Kocha Kim Paulsen
Manara: Fiston, Aucho na Djuma hawatacheza