Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wa pili wa Ligi Kuu msimu huu 2021/22, kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Simba SC wamepoteza mchezo huo ugenni mjini Bukoba mkoani Kagera, huku bao la wenyeji likipachikwa wavuni na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Khamis Kiiza Diego.

Mchezo wa kwanza kwa Simba SC kupoteza msimu huu ulikua dhidi ya Mbeya City FC na baada ya hapo walilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Mtibwa Sugar.

Hata hivyo Kagera Sugar wamemaliza dakika 90 wakiwa pungufu, kufuatia mfungaji wa bao lao la ushindi Khamis Kiiza kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 89.

Kwa matokeo hayo Simba SC inaendelea kusalia na alama zake 25 ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, huku Kagera Sugar wakisogea hadi nafasi ya 9 wakitokea nafasi ya 11 kwa kufikisha alama 16.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na alama 35, tofauti ya alama 10 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC ambao ni mabingwa watetezi.

Ahmed Ally awatuliza mashabiki Simba SC
Majaliwa - Watanzania tushikamane kuipa thamani Tanzanite