Uongozi wa Simba SC umempa Baraka zote Kocha Msaidizi kikosi cha Klabu hiyo Seleman Matola, aliyeamua kwenda kuongeza ujuzi kupitia Kozi maalum ya Ukocha.

Matola alithibitisha kuondoka Simba SC kwa kipindi kifupi kwa ajili ya kwenda kusomea Leseni A, itakayompa fursa ya kuwa Kocha Mkuu kwenye timu yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally, amesema Uongozi wa Klabu umepa Baraka zote Matola na umemtakia kila la kheri katika Masomo yake.

Ahmed amesema kuondoka kwa Kocha huyo mzawa ni mpango ambao ulifahamika mapema na wala hakuna msuguano wowote uliojitokeza baina ya Uongozi na muhusika.

“Hakuna tatizo lolote ambalo lipo na tunajua kwamba Matola amepata fursa ya kwenda kusoma hili ni jambo jema na zuri kabisa.”

“Uongozi umebariki suala la yeye kwenda kusoma na kuhusu kurejea kwenye nafasi hiyo ni mpaka pale ambapo atakamilisha masomo kwani kwa sasa bado ni mapema kuzungumzia hilo.” alisema Ahmed Ally

Hadi sasa Uongozi wa Simba SC haijatangaza Kocha Msaidizi atakaeyeziba nafasi ya Matola ambaye alionekana kuwa msaada mkubwa wa Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.

Kelvin Mandla: Simba SC ni kubwa Afrika
Meddie Kagere: Young Africans imeimarika