Klabu ya Simba SC imepigwa faini ya Randi za Afrika Kusini 162 000 sawa na Dola 10,000 za Marekani (Tsh Milioni 23.25) kwa kosa la kuwasha moto katika eneo la kuchezea mpira katika dimba la Orlando Pirates.

Wachezaji wa Simba SC walizunguka duara katikati ya uwanja na kuwasha moto na kuanza kufanya maombi yao.
Klabu ya Orlando Pirates ilituma barua ya malalmiko CAF juu ya wageni wao kuwasha moto uwanjani na kuwaharibia uwanja wao.

Msimamizi wa mechi nae katika taarifa yake aliandika kuwa Simba walifanya tukio hilo katika uwanja.

CAF baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha na kuikuta klabu ya Simba SC ikiwa na makosa imewapiga faini ya $ 10000 sawa na Milioni 23.23 za Kitanzania kwa kosa hilo.

Kiasi hicho kinatakiwa kilipwe ndani ya siku 60.

Simba pia inaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku 3.

SOURCE : CAF

TBS yawataka watoa huduma kuhakiki vipimo
TPBL yafanya maboresho Ratiba ya Ligi Kuu