Rais wa Heshima na Mwekezeji wa Klabu ya Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ ameonesha furaha yake baada ya kikosi cha Klabu hiyo kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Singida Big Stars.

Dewji ameonesha furaha hiyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, akiweka video ya magoli ya Simba yaliyofungwa na Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho.

Mbali na kuweka Video hiyo, Tajiri huyo ameandika: Napenda jinsi Simba inavyocheza na kufunga! Tupo tayari kwa ajili Ligi ya Mabingwa #NguvuMoja

Simba SC itaanza kampeni ya kucheza hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwishoni mwa juma lijalo kwa kucheza ugenini (Guinea) dhidi ya Horoya AC.

Simba SC imepangwa Kundi C sambamba na Mabingwa wa Uganda Vipers SC, Raja Casablanca (Morocco) na Horoya AC.

Ratiba ya Bunge yashtua kutotaja Muswada wa Sheria ya Habari, TEF yawatuliza wadau
Abutwaleeb Mshery kutubiwa Tunisia