Klabu ya Simba imemtangaza Didier Gomes Da Rossa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Gomes ambaye anachukua nafasi ya Sven Vandebroeck aliyeachana na klabu hiyo hivi karibuni, alikuwa kocha mkuu wa timu ya Al Mereikh ya Sudan.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mara baada ya kutambulishwa rasmi na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, Gomes amesema aliondoka El-Mereikh kutokana na maamuzi yake.

“Timu niliyoondoka niliamua mwenyewe, nataka kuwepo Simba kwa muda mrefu. Nina furaha sana kuwa hapa na tuna nafasi ya kufanya mengi pamoja mbeleni,” amesema kocha Gomes baada ya kutambulishwa,”.

Vikosi Libya vyagoma kuondoka
Meneja Tanesco atakiwa kujibu sababu kukatika kwa umeme