Kwa mara ya kwanza Uongozi wa Simba SC umeweka wazi namna ulivyokubaliana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ambaye kwa sasa yupo nchini kwao kwa mapumziko.

Simba SC ilimpa nafasi Morrison kurejea nchini kwao kwa ajili ya matatizo ya kifamilia, huku mkataba wake ukitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Barbara Gonzalez amesema mbali na Morrison kupewa nafasi ya kurejea nchini kwao Ghana, pia Uongozi wa Simba SC ulimpa wasaa wa kutafuta timu, kwani alifahamu hatokuwa sehemu ya kikosi kwa msimu ujao.

Amesema Simba SC ilifikia maamuzi hayo, kufuatia mwenendo wa kinidhamu wa mchezaji huyo kutokua mzuri hasa alipokua nje ya Uwanja.

“Tulimpa Morison Barua ili apate nafasi ya kutafuta timu, hakuwa kwenye mipango yetu tena kutokana na ripoti zake kujirudia rudia hasa zile za nje ya uwanja.. hata yeye alijua Simba SC hakuna nafasi ya kuongeza mkataba tena”

“Ni kweli ametuomba Barua ya kumuamuru aondoke, lakini bado yupo ndani ya mkataba na Simba SC, na kama anataka kuondoka kabla ya mkataba lazima afanye hayo maombi, ila utaratibu uliotumika sio sahihi, klabu ya Amazulu FC ilituambia inamuhitaji Rally Bwalya na tulifuata utaratibu, lakini kwa Morrison klabu anayotaka kwenda bado haijafahamika.”

“Nimemwambia Morrison mimi sina shida, ninahitaji kitu kimoja tu, waambie hiyo klabu watuandikie Barua, sina tatizo, kwa nini hiyo klabu inagoma kutuandikia barua ya kumuhitaji Morrison, kuna kitu hapa!”

“Simba SC hatuna tatizo, mimi nitakua wa kwanza kusema tunahitaji wachezaji wetu waendelee, wapate nafasi nyingi za kucheza nje ya Simba SC na nje ya nchi, lakini tunahitaji utaratibu wa maandishi na hii ipo kisheria, kama kuna mtu anataka kuondoka, ataondoka lakini kwa utaratibu.” Amesema Barbara

Morrison anadaiwa kufanya mazungumzo na Viongozi wa Young Africans, huku taarifa zingine zikieleza tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

Tetemeko laua watu zaidi ya 1,500
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 23 2022