Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ghana Kwesi Apiah, ili atue Msimbazi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Football Ghana 3, Simba SC imejipanga kumuajiri nguli huyo kama Mkurugenzi wa ufundi, ambaye atafanya kazi kwa karibu na Uongozi pamoja na Benchi la Ufundi la Klabu hiyo linaloongozwa na Kocha kutoka nchini Brazil Roberto Oliviera.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Simba SC kuhusishwa na Kocha Kwesi Appiah, kwani iliwahi kukaribia kumpa ajira ya kuwa Kocha Mkuu mwanzoni mwa msimu huu, lakini Kocha Zoran Maki alitangazwa kushinda Kinyanganyiro hicho.

Licha ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa nchini Ghana, Appiah anatajwa kuwa kwenye mpango wa kufukuzia ajira ya Kocha Mkuu wa Kikosi cha Ghana (Black Stars), ambayo kwa sasa haina mkuu wa Benchi la Ufundi, kufuatia kuondoka kwa Kocha Nana Otto Addo.

Kwesi Appiah anakumbukwa kwa kuiongoza Timu ya taifa ya Ghana, katika safari ya kufuzu Fainali za kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2014 Nchini Brazil.

Simba SC haijawahi kuwa na Mkurugenzi wa UFudi tangu ilipoingia katika mfumo wa mabadiliko, na mara kadhaa wadau wa soka wa klabu hiyo wamekuwa wakiutaka uongozi kumuajiri mtu huyo, ambaye atakuwa na jukumu zito la kufanya kazi za kiutendaji zinazohusu Ufundi.

Ibenge afurahia kucheza Dar es salaam
Ashuhudia jinsi alivyomdhibiti mumewe asichepuke