Ingawa sio rasmi lakini tumeona tuiwasilishe hapa kutokana na mchezo wa soka ambao kwa sasa unatamba duniani kufuatia kuwa sehemu kubwa ya kuingiza kipato katika taasisi mbalimbali za mchezo huo.

Ukurasa wa Instagram wa Sports Arena umeweka taarifa inayoainisha thamani ya vikosi vya klabu nne zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

Haijawahi kutokea kwa kuwekwa hadharani thamani halisi ya usajili wa vikosi vya klabu za soka Tanzania bara na hata huko Zanzibar, na ndio maana hii kwetu tumeipokea kama mawazo ya Sports Arena, japo wao wamethibitisha kuitoa kwenye mtandao wa transfermarkt.

Taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa Sports Arena inaeleza kuwa: Simba ndio klabu yenye thamani kubwa Tanzania ikiwa na thamani ya EURO Milioni 2.2 kulingana na mtandao wa transfermarkt.

Mabingwa hao wanashikilia Ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 3 mfululizo wanaongoza katika orodha ya thamani, ikiwa mbele ya mabingwa wa kihistoria Young Africans na Azam FC.

Utafiti huo umeangazia haki za kupeperusha matangazo, faida, umaarufu, uwezo kimchezo na umiliki wa uwanja.

Hivi hapa vilabu VITANO bora vyenye thamani kubwa VPL:

1. SIMBA SC – Sh 6.2 Bilioni (€2.20m)

2. YANGA SC – Sh 3.9 Bilioni (€1.38m)

3. AZAM FC – Sh 2.2 Bilioni (€750k)

4. MTIBWA SUGAR – Sh 1Bilioni (€375k)

5. NAMUNGO FC – Sh 560.8 milioni (€200k)

ASFC: KMC FC yaiwinda Dodoma Jiji FC
Tshabalala ashughulisha wadau mitandaoni