Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC, wanongoza kwa wastani wa wachezaji wenye umri mkubwa zaidi, miongoni mwa wachezaji wa klabu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu msimu huu 2020/21.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwanaspoti, Simba SC inaongoza kwa wastani wa kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa kwa kuwa na asilimia 26.96, ikifuatiwa na Tanzania Prisons.

Hata hivyo Mwanaspoti wametoa orodha ya timu za Ligi Kuu zinazoongoza kwa wastani wa kuwa na wachezaji wenye umri mdogo, ikiongozwa na Coastal Union yenye asilimia 22.42.

Fully Zulu Maganga wa Ruvu shooting na Agrey Morris wa Azam FC ndio wachezaji wenye umri mkubwa zaidi (36 yrs) Ligi Kuu Tanzania bara.

Shello Mussa wa Mtibwa sugar ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi (16 yrs) Ligi Kuu Tanzania bara.

Wastani wa umri wa wachezaji wa klabu ya Young Africans ni (24.9).

Timu (5) zenye wastani mkubwa wa umri

1. Simba sc = Wastani umri 26.96

2. Prisons = Wastani umri 26.62

3. Ruvu shooting = Wastani umri 26.4

4. Namungo = Wastani umri 25.48

5. Dodoma fc = Wastani umri 25.23

Timu (5) zenye wastani mdogo wa umri.

1. Coastal Union = Wastani umri 22.42

2. Mbeya city = Wastani umri 23.11

3. Ihefu fc = Wastani umri 23.21

4. Mwadui fc = Wastani umri 23.36

5. Biashara Utd = Wastani umri 23.38

Maelfu waandamana nchini Ufaransa
Jela miaka 20 kwa kukutwa na nyamapori