Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC watacheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba SC imepangwa na klabu hiyo, baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa faida ya mabao mengi ya mabao ya ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Simba SC itaanzia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Novemba 28, kabla ya kucheza mchezo wa mkondo wa pili nchini Zambia Desemba 05.

Mshindi wa jumla wa michezo hiyo, atatinga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho msimu huu 2021/22.

Michezo mingine ya hatua ya mtoano iliyopangwa leo Jumanne (Oktoba 26) majira ya mchana huko Cairo nchini Misri.

Drake amiliki cha kuazima.
Marekani yasitisha msaada Sudan